0
Afisa Elimu Vifaa Na Takwimu Halmashauri Ya Wilaya Ya Babati Abedi Mbaruku


 Wakati Shule Zinaendelea Na Usajili Shule Za Msingi Katika Darasa La Awali Na Kidato Cha Kwanza Kwa Shule Za Sekondari Walimu Wakuu Wameonywa Kuwatoza Wazazi Fedha Kwa Ajili Ya Michango.
Hayo Ameyaeleza Kaimu Afisa Elimu Idara Ya Elimu Msingi Halmashauri Ya Wilaya Ya Babati Mkoani Manyara Julius Sikay  Alipohojiwa Na WALTER HABARI Ambapo Amesema Kwa Sasa Muitikio Wa Wazazi Ni Mkubwa Katika Kuandikisha Watoto Tangu Serikali Ya Awamu Ya Tano Ilipoanza Kutekeleza Sera Yake Ya Elimu Bure [Elimu Bila Malipo] Kwa Shule Za Msingi Na Sekondari.
Siay Amesema Kwa Sasa Wanatarajia Kuvunga Lengo La Uandikishaji Kwa Kuwa Watu Wanaongezeka Hali Inayopelekea Kukosekana Kwa Madarasa Katika Baadhi Ya Shule.
Amesema Kwa Sasa Bado Wanatumia Takwimu Za Sensa Ya Watu Na Makazi Ya  Mwaka 2012 Lakini Inavyonekana Kwa Mwaka Huu Idadi Kubwa Ya Watoto Watasajiliwa Zaidi Akiongeza Kuwa Mpaka Kufikia Tarehe 23 Mwezi February 2018 Tumeshafikisha Asilimia 75% Na Idadi Hii Inaweza Kufikia Hata Zaidi Ya 100% Ifikapo Mwezi March.
WALTER HABARI Ilipomuuliza Kuhusu Kuzuiwa Kwa Michango Ambayo Mingine Inahusu Wanafunzi Kupata Chakula Cha Mchana Shuleni,Kaimu Afisa Elimu Alisema Rais Hajazuia Watoto Kula Shuleni Isipokuwa Alichosema Ni Utaratibu Gani Utumike Badala Ya Utaratibu Wa  Wazazi Kuchangia Yeye Amekazia Kwamba Sasa Sio Wazazi,Kwa Hiyo Sisi Tumelipokea Hivyo  Na Tunataraji Hata Wazazi Watakuwa Wamelipokea,Itakuwa Sio Wazazi Tena Ni Jamii Itakuwa Inachangia Ili Kuondoa Kero Kwa Wazazi.
Ameongeza Kuwa Wanafunzi Watakuwa Wanakula Shuleni Lakini Hatujajua Watatumia Mfumo Gani Na Kwamba Wanasubiri Muongozo Kutoka Juu.
Amesema Katika Shule Za Msingi Halmashauri Ya Babati Hawatarajii Wanafunzi Kufukuzwa Sababu Ya Michango Au Chakula Kwa Kuwa Rais John Magufuli Ameshatoa Tamko Hilo.
Akielezea Takwimu Katika Shule Za Msingi 138 Za Serikali Na Tano [5] Za Binafsi Afisa Elimu Vifaa Na Takwimu Halmashauri Ya Wilaya Ya Babati Abedi Mbaruku Amesema Katika Makisio Walitarajia Kuandikisha  Darasa La Awali Wanafunzi 10,952 Wavulana 5,433 Na Wasichana 5519 Ambapo Mpaka Kufikia Tarehe 23.1.2018 Walioandikishwa Ni Wavulana 4,799,Wasichana 4,624 Jumla 9,423 Awali Tofauti Ya 1,529.
Mbaruku Amesema Wa Kuwa Bado Zoezi La Uandikishaji Linaendelea Mpaka Mwishoni Mwa Mwezi Februari Wanararajaia Idadi Waliotarajia Ikazidi.
Kwa Upande Wa Darasa La Kwanza  Halmashauri Ilikusudia Kuandikisha Wavulana 6,422 Na Wasichana 6,421 Jumla 12,843 Lakini Mpaka Kufikia January 23 Mwaka Huu Wameandikishwa Wavulana 6278 Na Wasichana 6131 Na Kufikisha Jumla Ya Wanafunzi 12,409 Tofauti Ya Watoto 434.
 Afisa Takwimu Amesema Kuwa  Idadi Hiyo Ni Ndogo Lakini Matumani Yao  Mpaka Kufikia Mwishoni Mwa Mwezi February Watakuwa  Wamewasajili  Watoto Hao Zaidi Ya  434.
Akizungumzia Tofauti Ya Mwaka Jana Na Mwaka Huu Ameeleza Kuwa Kwa Mwaka Jana Idadi Ilikuwa Kubwa Kwani  Waliandikisha Wanafunzi Wa Darasa La Awali 13,519,Darasa La Kwanza 14,737 Ikichagizwa Na Elimu Bila Malipo.
Amesema Kwa Kuwa Elimu Bila Malipo Ilianza Rasmi Mwaka Jana,Kuna Uwezekano Watoto Wakaandikishwa Wengi Zaidi.
Amewataka Wazazi Na Walezi Wawapeleke Watoto Shule Kwani Hizi Sio Zama Za Kuficha Mtoto Kwa Madai Kuwa Hauna Uwezo Kuna Methali Inayosema Ukiona Elimu Ni Ghali Jaribu Ujinga,Lakini Kwa Kuwa Mmeambiwa Elimu Ni Bure Wapekeni Wakapate Elimu Iwasaidie Baadaye.
Aidha Amewataka Walimu Wakuu Ambao Ndio Watendaji Wawapokee Wanafunzi Bila Kujali Idadi Yao Kwani Hilo Sio Jukumu Lao,Shule Za Msingi Hatujazi Tunapokea Watoto’.Alisema Mbaruku.
Pia Amesema Wazazi Wasiangalie Kimo Au Umbile La Mtoto  Bali Waangalie Umri Kama Unaruhusu Kupelekwa Shule.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top