
Biashara imefanikiwa kupanda baada ya kuitwanga Transit Camp kwa mabao 3-2 katika mechi kali mjini Musoma.
Ushindi huo unaifanya Biashara kufikisha pointi 30 na kubaki kileleni mwa Kundi C ikifuatiwa na Alliance.
Wenyeji Biashara walilazimika kufanya kazi ya ziada kupata mabao ya haraka baada ya timu hizo kushindwa kufungana mapema.
Timu
nyingine nne zilizopanda Ligi Kuu Bara ni pamoja na JKT Ruvu iliyokuwa
ya kwanza, KMC ya Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance ya
Mwanza na Biashara.
Sasa imebaki timu moja inayotafutwa kukamilisha idadi ya timu sita zinazotakiwa kupanda ligi kuu msimu ujao.
Post a Comment
karibu kwa maoni