Usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 04, 2018 mtu mmoja
ambaye jina lake halijatambulika hadi sasa amejiua kwa kujipiga risasi nje ya
Ikulu ya Marekani mjini Washington.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Shirika la Habari la ABC umeripoti kuwa mtu huyo alikuwa karibu na geti la White House na alianza kufyatua risasi akielekeza Ikulu na kisha baadae kujipiga risasi mwenyewe.

Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump na Familia yake
hawakuwepo Ikulu wakati wa tukio hilo likitokea walikuwa mjini Florida ambako
imeelezwa walienda kupata chakula cha usiku.
Mashuhuda waliyokuwepo kwenye tukio hilo waliohojiwa na gazeti la Washington Post wamesema kuwa mtu huyo alikuwa kwenye msongamano wa watu na alizua taharuki baada ya kufyatua risasi.
Jeshi la Polisi mjini Washington tayari limetoa taarifa juu ya tukio hilo ambapo limedai kuwa mtu huyo amefariki dunia na hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa huku likikiri wazi kuwa jina la mtu huyo bado halijatambulika na uchunguzi unaendelea.
Rais Trump hadi sasa bado hajatoa tamko lolote hadi sasa ingawaje watalaamu wa Masuala ya Kidiplomasia na Siasa wanahusisha tukio hilo na mambo yanayoendelea ndani ya Ikulu ya Marekani.
Wiki iliyopita baadhi ya watumishi White House walijiuzulu kuhudumu baada ya kudai kuwa majukumu yao yanaingiliwa na mtoto wa kike wa Trump, Ivanka Trump na mumewe .

Post a Comment
karibu kwa maoni