Kijana
huyo amefanya tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na
matatizo na mkewe kuhusu suala la unyumba jambo ambalo lilimpelekea
kumrudisha mkewe huyo nyumbani kwa mama yake, ambapo amekaa huko
takribani wiki tatu, siku moja kabla ya kikao cha kuwasuluhisha wanandoa
hao ndipo kijana huyo ametekeleza mauaji hayo.
Mtoto
wa marehemu Elizabeth Simon (70) ambaye ni Mchungaji Ezekia Simon
amesimulia jambo hilo kwa undani zaidi na kusema kuwa chanzo cha yote
hayo kuwa ni matatizo ya unyumba na kudai kuwa kijana huyo ambaye yeye
ni shemeji yake alionekana amekuja na kusudio la kuwauwa wote yaani mama
yake pamoja na mdogo wake huyo ambaye amejeruhiwa tu.
"Kisa
cha kifo cha mama kimetokana na Mume wa dada kutoelewana katika habari
za unyumba. Walikuwa na mgogoro kwa maana hiyo ikapelekea kumfukuza
mkewe hivyo alikuja hapa yapata kama takribani wiki tatu yuko hapa
nyumbani na baada ya hapo mimi kama Mkuu wa familia nilijaribu kutafuta
njia ya kuwasuluhisha hivyo tarehe ambayo tulipanga kukutana ilikuwa
jana ingawa hatukufanikiwa kukutana baada ya mzazi wa kijana kusema
hakupata taarifa, matokeo yake yule kijana ndiyo amekuja akawashambulia
mama pamoja na dada na kusababisha mauti ya mama" Alisema Mchungaji
Simon na kuendelea;
"Yule
kijana alikuja kwa lengo la kuuwa wale na yeye kujiuwa kwa sababu
alipowashambulia na kuwajeruhi yeye alijimwagia Petroleum na kujichoma
moto ndani ya nyumba hii hii"
Post a Comment
karibu kwa maoni