Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema
amesikia malalamiko ya mwanamuziki Diamond lakini hawezi kumjibu kwa
sababu zipo taratibu za kufuata kama anaona hajatendewa haki.
Shonza
analijibu hilo ikiwa ni siku moja tangu mwanamuziki 'Diamond' amtaje
waziri huyo katika malalamiko yake, akidai amekuwa akikurupuka na
kutolea mfano wa kufungia nyimbo na wasanii wakati akihojiwa na kituo
cha redio cha Times.
Waziri
huyo amesema hayupo tayari kumjibu Diamond ingawa wasanii wanapaswa
kuelewa kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama msanii mkubwa namna
gani.
"Aliyewafungia
wasanii si Shonza bali ni mamlaka na kama mlivyoona safari hii hadi
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeingilia kati suala hilo, sasa
mtu anaporusha tuhuma kumlaumu Shonza atakuwa hanitendei haki. Isitoshe
ofisi zetu zipo wazi anayeona ameonewa afuate taratibu katika kudai haki
yake na si kulalamikia pembeni," amesema Waziri Shonza.
Kuhusu
kutoitwa kwa wasanii kabla ya kufungiwa kwa nyimbo zao Shonza amesema
hilo waulizwe Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) maana ndio wenye kujua
sababu na kwa baadhi ambao aliwaita ameeleza kuwa ni kutokana na kupewa
maagizo ya kubadilisha nyimbo zao na kuwahi kukiri makosa lakini
wakashindwa kutekeleza.
Katika
mahojiano hayo na redio Times, Diamond alielekeza mashambulizi zaidi
kwa Waziri Shonza na kudai kwamba amekuwa akifanya maamuzi yake kwa
kukurupuka akisahau kwamba viongozi hawana mchango wowote kwao na pia
wamekuwa wakiziumiza familia zao.
Februari
28 TCRA iliandika barua kwa vituo vya redio na televisheni ikiviagiza
visitishe kuonyesha nyimbo 15 za wasanii kadhaa kutokana na kuwa na
maudhui ambayo yanaenda kinyume na maadili na kanuni za Huduma za
Utangazaji(Maudhui) 2005.
Nyimbo
hizo na jina la msanii aliyeimba kwenye mabano ni Hallelujah na
Wakawaka (Diamond), Kibamia (Roma Mkatoliki), Pale Kati patamu, Maku
(Makuzi) na Mikono Juu (Ney wa Mitego), Hainaga Ushemeji(Manifongo), I
am Sorry JK(Nikki Mbishi.
Nyingine
ni Chura (Snura) na Nimevurugwa (Snura), Tema mate tumchape(Madee),
Uzuri wako(Jux), Nampa papa(Gigy Money), Nampaga(Baranaba) na Bongo
Bahati mbaya(Young D).
Post a Comment
karibu kwa maoni