0

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amewataka watendaji na wataalamu wa Mahakama, nchini kujitathmini na kuona namna wanavyoweza kutoa msukumo wa maboresho wa Mahakama katika suala la kutoa haki kwa wakati.

Jaji Prof. Juma amesema hayo Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa watendaji na wataalam wa Mahakama wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa mpango wa maboresho wa Mahakama nchini.

Jaji Mkuu huyo wa Tanzania amesema kuwa kuna tatizo la utoaji wa taarifa muhimu kwa Wananchi kitika Mahakama jambo linalowanyima wananchi haki ya kufuatilia mashauri yao.

Pia Jaji Mkuu amewataka watendaji kufanya Tathmini na kuona namna wanavyeweza kutoa msaada katika kufikia malengo yaliyokusidiwa na Mahakama.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top