Wafanyabiashara
na wawekezaji nchini wameeleza kero na changamoto wanazokutana nazo
katika uendeshaji wa shughuli zao, huku wakibainisha kuwa zimekuwa
zikirudisha nyuma dhamira ya Serikali katika kukuza sekta binafsi
nchini.
Wametoa
kauli hizo leo Jumatatu Machi 19, 2018 Ikulu Dar es Salaam katika
mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara, huku hoja zao
zikichukuliwa na mwenyekiti wa baraza hilo, Rais John Magufuli.
Kabla
ya kuanza majadiliano hayo, Rais Magufuli amesema leo utafanyika
mjadala wa kuleta mabadiliko ambapo kila mfanyabiashara atasimama na
kueleza kero na changamoto zinazomkabili, zitapatiwa majibu na watendaji
wa Serikali, wakiwemo mawaziri.
“Leo
kuna watu kama 13 kutoka Tume ya Mipango, nataka tuzungumze leo kwa
uwazi, mimi hata tungezungumza leo na kesho sawa tu tuendelee , nataka
mseme kwa uwazi, dakika tatu kila mmoja atazungumza , nataka tu-solve
problem sio kila mara tunakutana hapa tunajadili mambo yaleyale,”amesema
Rais Magufuli.
Mfanyabiashara
Mwita Gachuma kutoka Mwanza ndiye ameanza kufungua mjadala huo akitoa
kero mbili ikiwamo tozo kubwa zinazotozwa nchini ikilinganishwa na nchi
jirani kama Kenya.
“Kwa
nchi za jirani wanatoza kuanzia asilimia 11, 13, sisi (Tanzania)
tunatozwa asilimia 33, asilimia 15 tunatakiwa kurudishiwa lakini hata
hivyo haturudishiwi hiyo asilimia 15, hatua hiyo inaathiri hata mzunguko
wetu wa fedha,”amesema.
Mfanyabiashara
mwingine kutoka Geita aliyejitambulisha kwa jina moja la Sospeter
amezungumzia pia kero ya kodi katika usafirishaji wa bidhaa.
Amesema TRA imekuwa ikikadiria kodi kubwa tofauti na kiwango cha mzigo.
“Kwa
mfano gunia la kilo 100 unaambiwa ni zaidi ya kilo 100. Kwa hivyo
inaathiri sana na matokeo yake unajikuta mfanyabiashara unabeba mzigo
kidogo, kwa hiyo tunaomba ulitazame hilo,”amesema.
Post a Comment
karibu kwa maoni