Rais
wa Urusi, Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa
muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa wa
zaidi ya asilimia 76 katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika jana Jumapili,
Machi 18 nchini humo.
Akizungumza
katika mkutano wa kutangazwa mshindi, Putin alisema ushindi wake ni
matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake
huku akieleza kuwa huo ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na
kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza
umoja na mshikamano.
“Hadi
hapa sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba,
kuhusiana na unyekiti na serikali kwa ujumla. Nilikwisha sema awali
kwamba nafikiria suala hilo. Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa
undani, kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza,”
alisema Putin.
Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Putin alikwepa swali alilotakiwa kueleza kama atagombea katika muhula ujao pia.
“Kwangu
kile mnachotaka kuniuliza inakuwa kama mizaha Fulani hivi, hebu
tuhesabu, ina maana nitasalia madarakani hadi nikiwa na miaka 100?
Hapana hapana hapana.”
Ushindi
huu mkubwa ambao ulitarajiwa, umekuwa na ongezeko la kura
ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012. Ambapo mpinzani wa
karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin alipata asimilia 12.
Post a Comment
karibu kwa maoni