Akitoa semina iliyoandaliwa na kituo cha Sheria na haki za Binadamu [LHRC] kwa waandishi wa habari wa radio za jamii mkoani Dodoma Dokta Jesse amesema kuwa Njia ya Kutumia Kamati ya Wataalamu gharama yake ni ndogo kuliko kuitisha tena upya Bunge la Katiba Katika mafunzo hayo yalioyokuwa yanajenga uelewa kwa wanahabari kuhusu sheria ,haki za binadamu na mchakato wa katiba mpya pamoja na yaliyofanyika mkoani humo amesema suala la katiba ni muhimu kwakuwa ni jambo ambalo litatumika katika vizazi vingine pia.
Amesema kuwa kamati hiyo itakuwa na faida kubwa kwasababu itaangalia kilicho bora kwa kuzingatia Sera za Nchi pamoja na kupewa Hadidu za Rejea akitolea mfano nchi ya Kenya ambayo ilitumia njia hiyo ya kamati maalumu.
“Hii Kenya walifanya baada ya kuwa kuna draft ile ya wananchi unadraft ile ya serilaki wakatengeneza commete of expart wakawambia sasa nyie tunawapa hadidu za rejea muangalie mazuri yaliokopande zote mtutengenezee draft nzuri halafu tutaipeleka kwa wananchi kwa hiyo wale wana harmonize na kureconsile rasimu ya warioba na katiba inayopendekezwa na hata katiba hii ya 1977 itakuwana document mbayo itakuwa ni high Brid ina pande zote lakini hili nalo litakuwa ni utashi na nadhani hii ni approach ambayo nadhani Raisi wetu ataipenda na itapunguza garama yake itakuwa ndogo”Alisema Dkt Jesse
Ameongeza kuwa namna ya kuipata kamati hiyo ya wataalamu hao ni kuchagua watu wasioegemea upande wowote na wajiite jina ambalo wanaweza kutumia katika mchakato huo ili kuwapeleka wananchi kwenye kura ya maoni na kuipitisha kwa kuikubali au kuikataa baada ya kushirikisha rasimu za katiba zote.
Naye afisa msaidizi kutoka kitoka kituoa cha sharia na haki za binadamu waliowezesha mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kuchagua radio jamii kwa kuwa zinazosikilizwa zaidi na watu wa vijijini ili kupata uelewa juu ya mchakato wa katiba mpya.
Amesema kuwa watu wengi walioko vijijini hawajui masuala ya sharia na katiba lilikuwa ni jambo ambalo linapotea kwenye masikio ya watu hivyo wakaona ni vema kuibua kupitia waandishi wa habari ambao wanawagusa wananchi moja kwa moja.
Kwa upande wake Afisa msaidizi dawati la Katiba kuoka LHRC Wakili Fortunatha Mtwae amesema kuwa mchakato huo utaendelea tu endapo serikali itakuwa na sheria inayoongoza itakuwa wazi.
Nao waandishi wa Habari waliopatiwa mafunzo hayo wameeleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kupata uelewa na wataupeleka kwa wananchi.
Wakati Kituo cha sheria na haki za binadamu likifanya jitihada ili kupatikana kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikumbukwe kuwa Rais wa awamu ya Tano kwa sasa Dk.John Magufuli alishatangaza wazi kuwa suala la katiba mpya sio kipaumbele katika serikali yake.
Post a Comment
karibu kwa maoni