Mamlaka
ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano nchini Tanzania imekanusha kutokea kwa hali ya Kimbunga
"ELIAKIMU" katika maeneo yanayozunguka nchi na kudai Kimbunga hicho kipo
kwenye visiwa vya Madagascar.
Hayo
yamebainishwa na taarifa zilizotolewa hivi punde na kurasa rasmi za
mamlaka hiyo Machi 17, 2018 na kusema ni ukweli Kimbunga kinachojulikana
"ELIAKIMU" kipo eneo la Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madagascar
na kinaelekea Kusini mwa kisiwa hicho.
Aidha,
Mamlaka ya hali ya hewa imesema imefuatilia mwenendo wa Kimbunga hicho
tangu kilipojitokeza mapema mnamo Machi 15, 2018 majira ya saa 11
asubuhi na kutoa utabiri wa hali ya hewa nchini kwa kuzingatia mifumo
yote ya hali ya hewa inayojitokeza.
Kwa upande mwingine, mamlaka hiyo imesema itajitahidi kutoa taarifa na tahadhari za utabiri kadri inapobidi kufanya hivyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni