0
Wakati hatua ya sita bora ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa Manyara ikiwa imesogezwa mbele kutokana na mvua inayoendelea kunyesha mkoani hapa uongozi wa timu ya Babati Mashujaa (BM Sc) imeibuka na kusema ratiba ya hatua hiyo ilikuwa inazibeba baadhi ya timu huku wao wakiwa wamebanwa.
Awali hatua hiyo ya sita bora ilikuwa ianze leo katika uwanja wa chuo cha ufundi Nangwa uliyopo Katesh wilaya ya Hanang lakini kutokana na hali hiyo ya  mvua kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Manyara (MARFA) imeamua kuisogeza mbele hili kutafuta uwanja mzuri katika wilaya nyingine.
Babati Mashujaa wanalalamikia ratiba ya awali kabla ya ligi kuhairishwa  katika hatua hiyo ya sita bora iliyokuwa inaonyessha wanacheza machi 21 na Usalama sc, alafu tena wanacheza machi 22 na Morning Star fc mechi zote hizo zinachezwa saa nane.
Akiongea na WALTER HABARI mwenyekiti wa timu ya soka ya Babati Mashujaa ( BM Sc) Madaraka Said alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa ratiba hiyo kwani inaonyesha watacheza mechi mbili mfululizo saa  nane bila kupumzika wakati timu zingine kwao ni tofauti.
Alisema katika hatua ya makundi ilikuwa hivyo hivyo wakalalamika kwa kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Manyara (MARFA) ambao ilikiri kufanya makosa na kuwahidi kurekebisha lakini cha ajabu na katika hatua ya sita bora mambo yamekuwa tena yale yale.
"Tuna wasiwasi na kamati ya mashindano kwani inaonekana wanapanga matokeo na tayari kama kuna timu wanaiandalia mazingira ya kuwa bingwa sisi hatutokubali tutawasiliana na uongozi wa chama cha soka mkoa wasipotusikiliza tutaenda hata TFF" alisema Said.
"Sisi tunachokata mpira uchezeshwe kwa haki kuna vijana wanataka vipaji vyao vikue hili mwisho wa siku wailetee heshima mkoa wetu lakini kwa mtindo huu tuna didimiza soka letu wenyewe" alisema Said.
Kwa upande wake katibu wa kamati ya mashindano wa chama cha soka mkoa wa Manyara ( MARFA) Yusuph Mdoe alisema ni kweli ratiba ilikuwa inaonyesha hivyo lakini ni makosa si ambayo yalijitokeza wakati ya uchapishaji huku akiahidi kuifanyia marekebisho.
"Si kwamba sisi tuna zibeba vilabu vingine hapana kila timu inapambana kwa uwezo wake mwenyewe ukishinda ushinde kialali kwani tunataka timu bora itakayokwenda kutuwakilisha Manyara katika ligi ya mabingwa mikoa kwa hiyo ratiba hiyo tutaifanyia marekebisho"alisema Mdoe.
Taarifa ambazo WALTER HABARI imezipata kutoka kwa moja ya kiongozi wa timu inayoshiriki ligi hiyo ameeleza kuwa kwa sasa ligi hiyo imehamishiwa wilaya ya Mbulu kutokana na Uwanja wa Nangwa wilaya ya Hanang uliokuwa ukitumika kujaa Maji. 
Taarifa kutoka katika chanzo hicho imedai kuwa ratiba hiyo itaanza jumapili march 18.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top