Mamlaka jijini Kigali nchini Rwanda imepiga marufuku matumizi ya vipaza sauti vinavyotumika kutoa adhana kwenye misikiti.
Hatua
hii imekuja wiki mbili baada ya mamlaka jijini Kigali kuyafunga
makanisa zaidi ya mia saba. Pia baadhi ya makanisa yalifungwa kwa sababu
ya kutokuwa na usajili.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mshauri mkuu wa mufti wa Rwanda Sheikh
Mbarushimana Suleiman taarifa hiyo imepokelewa na kilichopo sasa
wameanza kuifanyia kazi.
Sheikh
Suleiman amefafanua kuwa Kama vile yalivyofungwa makanisa zaidi ya mia
saba wiki mbili zilizopita jijini kwa ajili ya kelele huenda hii ni
ishara kwamba hata misikiti ikafutia endapo wenyewe watashindwa kuridhia
agizo hilo.
Lakini
kufuatia agizo lililotolewa na mamlaka ya tarafa ya Nyarugenge mjini
Kigali ambalo ni moja ya eneo lenye waislamu wengi, inawezekana sasa
sauti za adhana zisisikike kwa upeo wa juu.
Katibu
mtendaji wa tarafa hiyo Havuguziga Charles amefafanua kwamba hatua hii
imechukuliwa kwa sababu ya kelele zinazodaiwa kuwasumbua wananchi.
“Baada
ya kutathmini tatizo la kelele zinazowasumbua wananchi wakati wa ibada
makanisani iliamuliwa kwamba hata vile vipaza sauti vilivyoko juu ya
misikiti ambavyo waislamu hutumia wakati wa ibada kwamba vikome.
Tuliwaomba viongozi wa misikiti kwamba watafute njia mbadala za
kuwataarifu waumini wao saa za ibada bila kutumia vipaza sauti kwa
sababu vinasababisha kelele.,” amesema Nyarugenge.
Hatua
hii imejiri wiki mbili baada ya kufungwa makanisa zaidi ya mia saba
jijini Kigali kwa tuhuma hizo huku hata baadhi ya wachungaji wakiendelea
kuzuiliwa kwa shutuma za kukaidi agizo hilo.
Post a Comment
karibu kwa maoni