Benki ya NMB Mkoani Manyara Tawi la Babati imetoa msaada wa
Meza na Viti 47 kwa Chuo cha ualimu Mamire Kilichopo Wilayani Babati Mkoani
humo.
Akikabidhi Viti hivyo chuoni hapo vyenye thamani ya
shilingi million 5 Meneja wa Benki hiyo kanda ya Kaskazini Stratton
Chilongola alisema Masada huo ni kama sehemu ya ushiriki wao katika maendeleo
ya Jamii.
Alisema wamekuwa wakishiriki katika mambo mbali mbali
ikiwemo kutoa vifaa vya shule kwenye shule zenye mahitaji pamoja kutoa
misaada hospitalini na kwenye Maafa kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa
Wananchi ambao pia ni wateja wao.
Alisema wao kama benki wanahakikisha Kuwait wanasaidiana na
serikali kutatua changamoto ambazo zinaikumba sekta ya Elimu na hivyo ili
kufanikisha hilo benki ya NMB imetenga zaidi ya shilingi Billion 1 ili
kusaidia jamii katika sekta za elimu na Afya kwa mwaka huu wa 2018.
"Tunataka na
sisi tuwe chachu ya maendeleo ya Watoto wetu, hawa walimu ndio watakao
tufundishia watoto wetu tusiwaache wasome katika mazingira magumu,
tuwatengenezee mazingira ambayo wataifurahia fani yao ya uwalimu"
"Nawapongeza kwa juhudi zenu za kuhakikisha kuwatafuta wafadhili wa
kuendelea kusaidia mambo mbali mbali katika chuo hiki ili kuhakikisha Walimu
wetu watarajiwa wanatoka katika mazingira magumu '' alisema chilongola.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi
alisema Elimu ina manufaa kwa anayeipata na jamii nzima, hvyo kuwasaidia
wanafunzi hao ili wasome katika mazingira bora ni njia moja wapo ya
kuwatengenezea maisha bora wao na Taifa.
"Nawapongeza Benki ya NMB
pamoja na uongozi wa chuo kwa kutafuta wadau mbalimbali wa kuchangia Elimu,
Serikali haiwezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja, hvyo kwa kushairikiana
na wadau mbali mbali wa Elimu tunaweza kupiga hatua kubwa katika sekta hii ya
Elimu "alisema Mushi.
Aidha aliwataka Wanafunzi hao kuepukana na mambo
mbali mbali ya ovyo ambayo yanaweza kuharibu Sifa zao na sifa za chuo hicho
na badala yake kujikita katika masomo na kukumbuka kuwa wao ni walimu
watarajiwa.
|
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
karibu kwa maoni