Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amekutana na wajumbe
wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa ukuta unaozunguka machimbo ya
madini ya Tanzanite Mererani, Wilayani Simanjiro. Ukuta huo
unatarajiwa kuzinduliwa na rais John Magufuli mapema mwezi Aprili.
Kikao
hicho kilichoanyika jana Machi 18, 2018 kiliudhuriwa na Watumishi
kutoka Wizara ya Madini, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na
Makamanda kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Akizungumza
katika kikao hicho Prof. Msanjila amelipongeza Jeshi kwa ujenzi wa kasi
wa ukuta huo na kuongeza kuwa ilikuwa ni kazi ya kujitolea na jeshi
limeisimamia vizuri.
Kwa
upande wake, Naibu Kamanda wa Oparesheni ya ujenzi wa ukuta huo, Luteni
Kanali Rashidi Kanole amesema kuwa, siri ya ujenzi wa ukuta kuchukua
muda mfupi tofauti na muda wa utekelezaji wake, pamoja na mambo mengine
umetokana na kufanya kazi kwa kuzingatia utamaduni wa jeshi
unaohusisha kiapo na uzalendo na kutafuta mbinu za changamoto bila
kusubiri viongozi wa juu kwenda kutatua changamoto hizo.
Ujenzi wa ukuta huo ulipangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita lakini umekamilika ndani ya kipindi cha miezi 3.
Sambamba
na kikao hicho, pia, Prof. Msanjila amekutana na wadau wa madini
wilayani humo kujadili masuala mbalimbali kuhusu biashara ya madini
hayo mara baada ya ukuta wa kuzinduliwa.
Miongoni
mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na ulinzi shirikishi wa ukuta huo,
biashara ya Tanzanite, uwazi wa biashara na suala la vitambulisho vya
Taifa.
Kuhusu
vitambulisho Prof. Msanjila amesema kuwa atakayeingia ndani ya ukuta
huo ni yule tu atakayekuwa na kitambulisho cha Taifa.
Aidha,
pande zote mbili Serikali na wadau wamekubaliana kukutana tena ili
kujadili kwa kina suala la biashara ya madini hayo mara baada ya ukuta
kuzinduliwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni