Leo March 24, 2018 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu
ametoa ufafanuzi kuhusu utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa
kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo
imesambaa imekuwa na makosa.
Semakafu amesema
kuwa yametokea makosa wakati wa uandishi ila kujiunga na masomo ya
kidato cha tano na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo
inasomekana katika taarifa iliyotolewa jana.
“Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi” -Dkt. Semakafu
Post a Comment
karibu kwa maoni