Serikali
kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni
Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imesema imewaita wahusika wa
gazeti la Tanzanite ambalo limesambaa mitandaoni likiwa limebeba katika ukurasa wa mbele habari inayomhusu Mange Kimambi.
Katika
taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dkt Abbas amesema
kuwa, amelazimika kuwaita wahusika hao ambao atakutana nao leo ili aweze
kusikiliza upande wao baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu maadili
ya kitaaluma ya gazeti hilo.
Nakala
ya gazeti hilo linaloonekana mitandao linaonyesha kuwa lilipaswa
kutoka Machi 5, kwani hata usajili wake ni wa mara moja kwa wiki (kila
jumatatu).
Post a Comment
karibu kwa maoni