Mkuu wa wilaya ya Hanang Sara Msafiri katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani amekemea wanawake wilayani humo na mkoa kwa ujumla kuwa kama chambo cha kutumika katika migogoro inayoendelea wilayani humo.
Alisema wanawake wamekuwa wakitumika katika migogoro
mingi ya vijiji na jamii katika wilaya
ya hanang na mkoa wa Manyara kutokana na mila na desturi walizorithi kutoka
enzi za mababu.
Alibainisha hayo katika
mahojiano maalum na WALTER HABARI kuhusu kuelekea siku ya wanawake duniani (Leo)
ambapo aliwataka wanawake wa wilaya hiyo kubadilika na kuachana na mkila potofu
na badala yake kujihusisha na masuala ya kimaendeleo.
Alisema kutokana na mila na desturi za makabila kutoka
wilaya ya Hanang na mkoa wa Manyara kwa ujumla kuna mila zinazofanana ambapo wanawake
wamekuwa wakitumika sana kwenye maandamano na migomo.
“Kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama
wa wilaya hii nimeshuhudia migogoro mingi inayotokana na chimbuko hilo la mila
na desturi, mila ambazo zimepitwa na wakati kwenye vijiji au jamii wanawake
wanatumika”.Alisema.
Akitolea mfano wa wanawake waliowahi
kaa nje kwa mgomo kuhusu matumizi ya ziwa Bassuto ambapo wapo wananchi
wanaoamini kuwa ziwa hilo kuabudu kwa masuala ya kimila na wapo wanaokuwa wanataka
matumizi ya ziwa hilo kwa masuala ya kiuchumi, Uvuvi na umwagiliaji ambapo wanawake
hao waligoma na kulala nje kwa muda wa miezi mitatu.
“Nikiwa nimeteuliwa kushika nafasi
hii mwaka 2016 nikakuta wanawake hao wameshakaa nje miezi mitatu katika kipindi
cha baridi cha kipimajoto 684 wanawake walikuwa wakikohoa huku wanaume wakiwa
majumbani kwao wanawatuma wanawake hao kugoma” Alisema.
Aliongeza kueleza kuwa migogoro
mingine imeshawahi kutokea katika maeneo
ya shughuli za uchimbaji wa madini na mgodi wa chumvi wa Gendabi wanawake zaidi
ya 400 walishawahi kukaa nje zaidi ya wiki tatu kugoma na hawataki kufuata
taratibu mbalimbali za kusikiliza kero zao katika vikao huku wanaume wakiwa
majumbani kwao.
Aliwaasa wanawake wote wa wilaya ya
Hanang na mkoa wa Manyra kuelekea siku ya mwanamke duniani kujielekeza nguvu zao
katika shughuli za uzalishaji za kijamii ili kukuza kipato na kusomesha watoto
wao badala ya kutumiwa kama chambo cha kuhamasisha maandamano.
Pia wanawake hao wahakikishe kuwa
wanapata haki ya kumili ardhi,mali na kwamba wasitumiwe tu akawa kama mtoto wa
kwanza katika familia kwani kuna kesi nyingi zinazobainisha wanawake wanaachika
katika ndoa zao wakiwa na watoto wanaowatunza bila kuachiwa chochote cha
kurithi.
“Pale ndoa zinapovunjika mwanamke
upate haki zako katika vyombo vya sheria, katika dawati la jinsia na kupata
ushauri katika ofisi za mkuu wa wilaya
na taasisi za kisheria zinazosaidia wanawake.”
Aidha aliwaasa kubadilika na
kujielekeza katika uzalishaji na kuacha kutumiwa kama chombo cha kufanya migomo
isiyo na tija.
Post a Comment
karibu kwa maoni