Katika kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda katika serikali ya awamu
yatano inayoongozwa na Rais John Pombe Magugufuli wanawake wilayani Babati
wameonyesha kuwa wanaweza hata bila kuwezeshwa baada ya kujikita katika kilimo
cha Pamba ambacho hakipatikani katika wilaya nyingine Mkoani Manyara.
Kilimo cha pamba katika mkoa wa Manyara kinafanyika katika kata tarafa ya
Mbugwe pekee.
Wakina mama waliojitokeza katika kilele cha sherehe za wanawake duniani
zilizofanyika katika kata ya Mwada kijiji cha Mbuyu wa Mjerumani katika taarifa
yao iliyopsomwa na Afisa Maendeleo ya jamii Priska wameelezea shughuli
wanazozifanya na changamoto wanazokabiliana nazo.
Akizungumza na mamia ya wakina mama waliojitokeza
kuadhimisha siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika katika kata ya Mwada kijiji
cha Mbuyu wa mjerumani Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi ameahidi
kuwapatia mitaji na mikopo wanawake wanaojishughulisha na ujasiaria mali katika
wilaya yake.
Awali mkuu wa wilaya Mushi alitembelea mashamba ya vikundi vya wakina mama
wa Mwada wanaojishughulisha na kilimo cha Pamba ambapo aliwahidi kuwa serikali
itawatafutia ardhi ili waweze kuendeleza kilimo hicho cha Pamba.
Kauli mbiu ya wiki ya wanawake mwaka huu kitaifa'KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA
TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJNI.'
Post a Comment
karibu kwa maoni