Muigizaji
wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu,
amefunguka na kudai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameletwa
duniani na Mungu kwa lengo la kusaidia watu nasio vinginevyo.
Wema
ametoa kauli hiyo mara baada ya Mhe. Makonda kuonesha nia ya kumsaidia
kumsafirisha kijana Ahmed Albaity kwenda nchini China kwa lengo la
kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa aliokuwa nao wa kupooza mwili mzima.
"Nikisema
'RC' wangu ni mtumishi wa Mungu basi namaanisha, mimi 'sometimes'
nasema uliletwa duniani kuja kufanya ya Mola wako tu. Mungu azidi
kukubariki 'my RC you are just like a guardian angel', ipo siku
wataelewa tu. 'I got a Good Feeling about Ahmed and Inshallah God will
work a miracle, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho", amesema Wema
Sepetu.
Kijana
Ahmed Albaity alipooza mwili wake mnamo 2007 baada ya kucheza vibaya
michezo ya kujirusha 'dive' katika bahari na kwa bahati mbaya alikosea
na kujipiga kichwa chini ambapo ilipelekea kupata matatizo yote hayo
mpaka sasa.
Post a Comment
karibu kwa maoni