0
Mahakama Kuu Kanda ya Dsm imepanga tarehe ya kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe dhidi ya jeshi la polisi ambapo itatangazwa Aprili 5.
Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari, ACT Wazalendo ndg Abdallah Khamisi, imesema kuwa Chama hicho kilifungua  kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yao ya kichama.

Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari,  Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

Hivi karibuni Msafara wa ACT Wazalendo ukiongozwa na kiongozi wa chama mkoani Morogoro uliripotiwa kuzuiliwa kwa muda kufanya shughuli zao za kichama katika kata wanazoziongoza.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top