0
Watu 12 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajari ya basi la kampuni ya City bus lililogana uso kwa uso na fuso katika kijiji cha makomelo wilayani Nzega mkoani TABORA.

Ajari hiyo imetokea usiku wa kuamkia Leo katika kijiji hicho baada ya kudaiwa dereva wa fuso kutaka kukwepa shimo na kujikuta fuso hilo likimshinda,hivyo  kupelekea kugongana uso kwa uso.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo .
Kamanda wa polisi kikosi cha usalama Bara barani mkoa wa Tabora  Inspekta Hardson,amesema
"Nimefika eneo la tukio SAA 2330hrs toka Tabora mjini 200kms. Eneo ni Makomero tarafa na wilaya Igunga mkoa wa TABORA.

"Gari T486 ARB FUSO ikiwa na mzigo wa viazi ikitokea Singida kuelekea Igunga tairi ya kulia litumbukia katika mashimo mawili barabarani kisha kupasua tairi na rim kupinda & mfumo wa usukani kukatika maungio ya steering rod na steering box kisha gari kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya City boy.

"Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha , 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya Igunga. 

"Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya Wilaya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi ambapo ME 02 wamepelekwa Bugando Mwanza na KE 01 amepelekwa Nkinga usiku .

"Dereva wa basi amefariki papo hapo. Wahusika wa FUSO kwa taarifa za awali inasemekana wamekimbia baada ya ajali hii."

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top