Aidha,
imeelezwa baada ya kuwachinja mapacha hao wenye umri wa miaka minne
Diocress alimkabidhi mwanawe mkubwa, Japhet Respicius (5) Biblia ili
awaombee marehemu kisha yeye kutoroka na sasa wanakijiji wenzake
wameazimia kumsaka.
Akizungumza
kwa niaba ya wanakijiji hao, afisa mtendaji wa kijiji cha Butayaibega,
Geofrey Deogratias alisema tukio hilo lilitokea saa saba usiku wa
kuamkia Jumapili.
“Nilifika
eneo la tukio na kukuta miili ya watoto Devotha Nyangoma Respicius (4)
na pacha mwenzake Johanes Kato Respicius (4) ikiwa imelazwa sebuleni
katika nyumba ya mtuhumiwa, huku vichwa vyao vikiwa pembeni mwa miili
hiyo” alisema.
“Huyu
mtuhumiwa alikuwa na watoto watatu ndani ya nyumba yake, lakini mtoto
mmoja Japhet Respicius (5) hakumuua na alishuhudia baba yake akifanya
unyama huo kwa wadogo zake.”
Mtendaji
huyo alisema baada ya kuona hali halisi alipiga simu polisi kutoa
taarifa juu ya tukio hilo, ambao walifika na kuichukua miili hiyo kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
Alisema
alipofika eneo la tukio alimkuta mtoto mkubwa akiwa nje ya nyumba
akilia, na kuwaeleza kuwa baada ya baba yao kuwachinja wadogo zake
alimkabidhi Biblia na kumsihi aendelee kuwaombea.
“Mtuhumiwa
baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kuelekea kusikojulikana,
lakini ameendelea kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa mwenyekiti wa
kijiji, mtendaji na baadhi ya wanafamilia” alisema mtendaji Deogratias.
Alisema
kuwa sehemu ya ujumbe huo ilisomeka: “Mwambie bibi Geogina ambaye ni
bibi wa mke wangu aitwaye Kokwenda David kuwa nimekwishatekeleza
alichokitaka kwa kuwaua Nyangoma na Kato, na mimi niko salama ila bado
nawatafuta wengine wawili ili niwaue na kujipeleka polisi mwenyewe,
msinitafute.”
Alisema
baada ya polisi kuchukua miili ya marehemu hao, mtuhumiwa alirudi tena
eneo la tukio akiwa na panga mkononi na kufyeka migomba yake na kuchoma
nyumba yake moto, huku akiwatishia ndugu na jamaa zake kuwa wakimsogelea
atawafyeka, na baadae alikimbia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Ollomi amesema baada ya msako mkali, mtuhumiwa ametiwa mbaroni jana Aprili 16 jijini Mwanza baada ya kutoroka na taratibu za kumsafirisha ili akabiliane na mashitaka zinafanyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Ollomi amesema baada ya msako mkali, mtuhumiwa ametiwa mbaroni jana Aprili 16 jijini Mwanza baada ya kutoroka na taratibu za kumsafirisha ili akabiliane na mashitaka zinafanyika.
Post a Comment
karibu kwa maoni