Mufti
wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) limefanya mabadiliko ya upatikanaji wa viongozi kwa
nchi nzima kuanzia ngazi ya Masheikh wa wilaya, mikoa na Taifa.
Akizungumza
jana Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya kikao cha Baraza
Kuu la BAKWATA kikao kilichokaa Mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi Machi,
Mufti alisema wamekubaliana kwa kauli moja kuwa upatikanaji wa viongozi
wa Kiislamu utakua ni wakuteuliwa na sio kuchaguliwa tena kama ilivyo
sasa.
Amesema
Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe Machi 31 - Aprili 1 umesema kuwa mfumo
wa uchaguzi hauwaachi watu salama sana sana husababisha migogoro ya hapa
na pale na makundi yenye kuleta chuki na kwamba mfumo wa kuteua ndiyo
mfumo wa kiislam
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA taifa Sheikh
Khamis Mataka amesema mbali na utaratibu huo wameanzisha mfumo mmoja wa
kukusanya mapato ili kukusanya fedha hizo kwa umakini tofauti na
ukusanyaji wa sasa ambao una mapungufu mengi na kupoteza baadhi ya
mapato.
Post a Comment
karibu kwa maoni