Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Jumatano Aprili 4, Mbowe amesema amenyang’anywa gari hilo tangu January, 2018.
“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu.” -Mbowe
“Lakini mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” amesema Mbowe bila kuelezea zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo.
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.
“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” -Kagaigai.
Post a Comment
karibu kwa maoni