Mbunge
wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza
mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye
amefanana naye akitajwa kumtelekeza.
Msigwa
amesema kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha
hivyo na anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa
walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kwa kutelekezwa,
asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.
“Ilikoanzia
imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho
nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu
yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni”, amesema
Peter Msigwa.
Hapo
jana Peter Msigwa ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook
akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo yupo na akithibitisha ni kweli
amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge wake alionao.
Post a Comment
karibu kwa maoni