Akizungumza
leo, Bungeni mjini Dodoma, Nasha amesema kuwa ukiruhusu hilo ni mwanzo
wa kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila na sheria zetu haziruhusu
ngono katika shule.
“Hata
sisi serikali kwa kweli hatupendi kusikia vitendo vya uonevu dhidi ya
watoto wa kike, kwasasa mfumo wetu wa elimu umepangwa katika namna ya
kuhakikisha wanafunzi wanaopata ujauzito wanapata fursa ya kusoma lakini
nje ya mfumo rasmi
"Kwahiyo
kuna fursa nyingine nyingi za kusoma kama nilivyosema katika swali
langu la msingi kupitia elimu ya watu wazima lakini vilevile vyuo vya
ufundi,“ amesema Nasha.
“Serikali
haitarajii na naomba niweke wazi wanafunzi ambao wamepata ujauzito kwa
njia yoyote ile hawataruhusiwa kuendelea na masomo kwasababu ukifanya
hivyo una halalisha na kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila zetu na
sheria zetu haziruhusu ngono katika shule za msingi na sekondari.“
Post a Comment
karibu kwa maoni