Kipindi cha TUZUNGUMZENA MANYARA FM kinachoendeshwa na John Walter na Lucas Mondu kimewakutanisha viongozi wakubwa wa CCM na CHADEMA katika kipengele cha Sikitiko Langu lililogusa viongozi wanaoahidi na kushindwa kutekeleza ahadi zao.
Akizungumza Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ccm [Taifa] Humphrey Pole pole amesema ni lazima wakuu wa wilaya,mikoa na watendaji wengine wa serikali kuhakikisha wanafanya ziara katika maeneo yao kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni agizo la mwenyekiti wa
chama Taifa Rais John Pombe Magufuli.
chama Taifa Rais John Pombe Magufuli.
Pole pole amewataka watanzania kuendelea kufanya siasa safi ili kuzidi kuendeleza amani iliyoachwa na waasisi wa taifa.
Kwa upande wa Amani Golugwa amefunguka na kusema kuwa viongozi wa Chadema wamefanya kazi kubwa ya kutekeleza yale waliyoyahaidi wakati wa kampeni huku akimmwagia sifa mbunge wa jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul kuwa ameyatekeleza yale aliyowaahidi wakazi wa Babati mjini.
Golugwa ameeleza kuwa kinachofanywa kwa sasa na Serikali ya awamu ya tano ni mipango ya awamu ya nne.
msikilize
msikilize
Post a Comment
karibu kwa maoni