Rais
John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya basi la
kampuni ya City Boy iliyotokea jana Aprili 4, 2018 katika Kijiji cha
Makomero Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora na kusababisha vifo vya watu
12.
Ajali
hiyo imetokea baada ya basi hilo lililokuwa limebeba abiria kutoka
Karagwe Mkoa wa Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso la
lori lililokuwa likitokea Singida kuelekea Igunga.
Taarifa
iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 5, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli mbali na kutoa pole,
amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama barabarani
kutafakari kwanini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo
yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza
maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.
Rais
amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kufikisha salamu zake
za pole kwa wafiwa wote na amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahala
pema peponi, majeruhi 46 wapone haraka.
“Nimepokea
kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 12
waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani jana usiku katika wilaya
ya Igunga mkoani Tabora, nawapa pole wafiwa wote, ndugu, jamaa na
marafiki walioguswa na msbia huu mkubwa,” amesema Rais Magufuli.
“Aidha,
nalitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa na
wilaya na mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani
kujitathmini na kutafuta majawabu ya kwanini ajali za barabarani
zinaendelea kutoka kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za
barabarani.”
Post a Comment
karibu kwa maoni