MAJIMBO ya Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni, Dar es Salaam leo
yamepata wabunge wapya baada ya waliokuwa wabunge wateule kuapishwa
bungeni mjini Dodoma.
Dk. Godwin Mollel ameapishwa kuwa Mbunge wa Siha, na Maulid Said Mtulia ameapishwa kuwa Mbunge wa Kinondoni. Wanasiasa hao wameapishwa wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 11 wa Bunge la Tanzania.
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amewapongeza wabunge hao na kuwatakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kabla ya kuuliza swali la nyongeza, Mtulia alisema, ana afya njema, akili timamu na yupo tayari kuwatumikia wananchi wa Kinondoni.
Mbunge huyo aliuliza Serikali ina mpango gani kuongeza barabara za lami kwenye jimbo hilo kutoka asilimia 10 ya zilizopo sasa ili zifikie angalau 50% ya barabara zote kwenye eneo hilo.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege amesema, Mtulia yupo katika nafasi sahihi, na amemkaribisha tena bungeni.
Mollel amewashukuru wananchi wa Siha kwa kumchagua tena, na amewaonya wanaompinga kwa sababu ya muda kuwa atawapiga kipigo ambacho hawajawahi kukipata.
Kandege amesema, Mollel yupo kwenye nafasi salama sana, kampongeza na kumkaribisha tena bungeni.

Post a Comment
karibu kwa maoni