Wanakijiji
2,510 wa kijiji cha Sangara kata ya Riroda wilaya ya Babati Mkoani Manyara
wanatarajia kuondokana na tatizo la maji pindi mradi wa maji wa shilingi
milioni 290,630,517 utakapokamilika.
Mkuu wa
wilaya ya Babati Raymond Mushi akizungumza katika majadiliano ya mradi huo wa
maji na usafi wa Mazingira katika kijiji cha Sangara amewataka wakazi wa kijiji
hicho kutunza mradi huo kwa uhai wa Binadamu na viumbe hai na wadau
waliofanikisha kila mmoja atimize wajibu wake ili mradi uendelee kuwepo.
Mradi huo
unaosimamiwa na wadau watano ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Babati
UTT-MFI,WATER AID TANZANIA,eWATER PAY LIMITED na HABITAT FOR HUMANITY TANZANIA
unatarajia kukamilika mwezi March 2019 kama anavyoeleza mkurugenzi wa WATER AID TANZANIA Dr. Ibrahim Kabole 'Tayari tumeshafanya utafiti na kubaini vyanzo vya maji lakini niwaombe wakaazi wa Sangara kutunza vyanzo vilivyopo ili kuepuka tatizo la maji'.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Martin Duuma Masong’ anaeleza kuwa kwa sasa wanafuata maji
umbali mrefu hivyo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.
Post a Comment
karibu kwa maoni