Mbunge
wa Ulanga (CCM), Gudluck Mlinga ameomba mwongozo wa Spika bungeni
akitaka kujua namna chombo hicho cha Dola kinavyoweza kuzuia wanawake
waliofika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai
ya kutelekezwa na watoto wao.
Mlinga
ameomba mwongozo huo leo Jumatano Aprili 11, 2018 akisema kitendo hicho
kinawadhalilisha watoto ambao hufika katika eneo hilo wakiwa na mama
zao, akidai kuwa kinavunja Katiba ya nchi.
Mwongozo
huo uliibua kelele bungeni baada ya mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga
kutoa majibu kwamba suala hilo ni la kisheria, kupingwa na wabunge
waliohoji sheria ipi.
Mlinga
alitaka kujua namna ambavyo Makonda anavyovunja Katiba kwa kuanika
mambo ya siri hadharani jambo ambalo linakwenda kinyume na Katiba,
akitaka Bunge liingilie kati na kukemea kitendo hicho.
Post a Comment
karibu kwa maoni