|
Afisa
Msajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndg. Godwill Mwamanga akizungumza na wanakijiji
wa kijiji cha Sanganjelu, wilayani Gairo akifurahia taarifa ya maendeleo ya mwitikio wa
wananchi Kushiriki Usajili ambapo aliarifiwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho kuwa mwitiko wa wananchi ni mkubwa.
|
Afisa Msajili wa
ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wilaya ya Gairo mkoani Morogoro Ndg.
Godwill Mwamanga ameeleza kuwa katika wilaya anayoisimamia zoezi la Usajili
linaendelea vizuri kutokana na wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi
jambo linaloonyesha matokeo chanya (asilimia kubwa) kufikiwa kwa NIDA kuweza
Kusajili idadi ya wananchi wenye umri wa miaka 18 na zaidi kama ilivyo lenga.
Akizungumza wakati
anatoka kituoni baada ya Kusajiliwa, Bi Fatma Mhando ameeleza amejitokeza na
kuwa mstari wa mbele kushiriki Usajili kutokana na kutofanikiwa kupatiwa mkopo
baada ya kutokuwa na Kitambulisho cha Kumtambulisha hivyo ‘nisingependa nifanye
makosa tena kwa kupuuzia fursa hii kwani ninaweza kukosa fursa nyingi mbeleni
za kuniinua kiuchumi n.k iwapo sitakuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Aidha Ndg. Mwamanga
ameeleza kuwa zoezi katika wilaya ya Gairo linatakiwa kufanyika katika kata
zote 18 ambapo hadi sasa wameshakamilisha katika kata 6: Msingisi, Rubeho, Chanjale, Iyogwe,
Italagwe na Mkalama. Kata mbili za Madenge na Leshata zoezi la Usajili linaendelea
na kutarajiwa kukamilika mwishoni mwa wiki ili kutoa fursa kwa wananchi wa kata
za Chakwale, Kibedya, Idibo, Nongwe, Mandege, Chagongwe, Ukwamani, Magoweko,
Ngiloli na Gairo ambazo bado kufikiwa kupata fursa hiyo.
|
Wananchi wa kijiji
cha Kinyolisi wakisikiliza maelekezo ya utaratibu wa Kusajiliwa kutoka kwa
Mwenyekiti (katikati) uliopangwa ili kila mwananchi anayefika katika kituo
hicho cha Usajili cha kijiji cha Kinyolisi asajiliwe kwa lengo la kupatiwa
Kitambulisho cha Taifa. Aidha Mwananchi mwenye fulana ya kijani kulia
amesitisha kuendelea kusuka na kukimbilia Kituo cha Usajili ili asikilize
maelekezo na kushiriki zoezi hilo kutokana na kutambua umuhimu wake kwa
maendeleo yake kama mwananchi wa Tanzania.
|
|
Maafisa
Usajili Wasaidizi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiendelea na
Kusajili wananchi wakazi wa kijiji cha Kilama kata ya Iyogwe wilaya ya Gairo mkoani
Morogoro katika kuingiza taarifa zao kwenye mfumo. Wananchi wengine pichani
wakiwa wameketi wakisubiri zamu yao ifike na kushoto Ndg. Ally John akiweka
saini ya kielektroniki kwenye mashine ya BVR.
|
|
Afisa
Msajili wa ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wilaya ya Gairo mkoani Morogoro akizungumza na baadhi ya viongozi na wasimamizi wa kijiji
cha Ngayaki kata ya Leshata juu ya maendeleo ya zoezi na changamoto zilizopo
ili zitatuliwe mapema alipofanya ziara kijijini hapo.
|
Post a Comment
karibu kwa maoni