0
Ni kupitia zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu linaloratibiwa na NIDA kwa kushirikiana na Uongozi wa mkoa hadi ngazi ya chini kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa/vijiji ambapo watendaji na wenyeviti wa mitaa/vijiji mkoani Morogoro katika wilaya zote wamejitoa vilivyo kufuata maelekezo waliyopewa kuhakikisha wanauhabarisha umma unajitokeza kwa wingi Kusajiliwa na Kutambuliwa kwa lengo la kupatiwa Kitambulisho cha Taifa.
Ameyasema hayo Afisa Msajili wilaya ya Morogoro Ndg. Sererya Wambura ambaye pia ni Msimamizi wa Usajili ngazi ya mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), alipokuwa anapitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa zoezi zilizowasilishwa ofisini kwake na kwa kupitia zilizoko kwenye mfumo akishirikiana na Afisa Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta wa NIDA Ndg. Rajabu Kabeya. Vilevile aliweza kujionea mwenyewe idadi kubwa ya watu katika vituo waliojitokeza Kusajiliwa wakati alipozuru vituo vya USajili katika wilaya mbalimbali za mkoa wa morogoro ambako zoezi linaendelea;Morogoro Mjini, Mvomero, Gaieo, Kilosa,Malinyi na Ulanga.
Aidha ametoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa mkoa wa Morogoro kwa jinsi ulivyotoa ushirikiano wa dhati wa hali na mali ikiwemo kutoa maelekezo kwa watendaji wa mitaa/vijiji kusimamia kwa karibu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuwa na Kitambulisho cha Taifa ili wajitokeze Kusajiliwa kwa wakati.
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu limeshafika katika mikoa yote nchi nzima ambapo NIDA ina ofisi katika kila wilaya hivyo wananchi wanapaswa kufika katika ofisi za serikali za mitaa/vijiji wanakoishi , kata ama ofisi za NIDA za Usajili wilayani kuulizia utaratibu wa hatua za kufuata ili wasajiliwe kwa lengo la kupatiwa Kitambulisho cha Taifa.
Wananchi wa kata ya Lukobe mtaa wa Mgudeni Ndg. Mana Zephurinus mwenye kilemba cheusi na Shani Ahmadi wakiwa katika Usajili hatua ya pili unaohusisha uchukuaji alama za kibaiolojia (picha, saini ya kielektroniki na alama za vidole).

Ndg. Thabit Salum Likanyaga Mwenyekiti Serikali Kilongo kata ya Mkundi akigawa fomu kwa wananchi wa mtaa wake ili waingie kwenye chumba cha Usajili hatua ya pili ya uchukuaji alamza kibaiolojia. Pamoja na kuwepo kwa mvua lakini wananchi waliendelea kusubiria huduma kutokana na kujua umuhimu wa Kusajiliwa ili kuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Wananchi Kata ya Kihonda Kaskazini, Mtaa wa Yespa katika pozi mbalimbali wengine wakijaza fomu, wakikagua fomu zao kama wamejaza inavyopaswa na wengine katika foleni kusubiria zamu yao ifike wasajiliwe hatua ya pili ya kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole na mashine maalum za NIDA - MEU
Maafisa Wasajili Wasaidizi Ndg. Alice Makarara aliyeketi na Ndg, Aziza Makoa wakitoa huduma kwa wateja waliofika ofisi ya wilaya ya NIDA ya Usajili Morogoro kuchukua vitambulisho vyao. Aliyeketi meza ya pembeni yao ni Ndg. Lucy Alphonce. Afisa Msajili Msaidizi wa NIDA akichakata taarifa za waombaji Vitambulisho vya Taifa Morogoro.

Afisa Msajili wilaya ya Morogoro Ndg. Sererya Wambura ambaye pia ni Msimamizi wa Usajili ngazi ya mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kulia akiwa pamoja na Afisa Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta wa NIDA Ndg. Rajabu Kabeya wakipitia ripoti za Usajili na Utambuzi wa watu za mkoa wa Morogoro ili kujua maendeleo ya zoezi.
Afisa Msajili wilaya ya Morogoro Ndg. Sererya Wambura ambaye pia ni Msimamizi wa Usajili ngazi ya mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akipokea hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Mteja mkazi wa mkoa wa Morogoro kuhusiana na zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu linaloendelea mkoani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top