Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, ametekeleza kwa
vitendo agizo alilopewa na Rais Magufuli, la kwenda kijijini Tundu,
Wilayani Mikumi kushughulikia kero ya mradi wa maji kijijini hapo.
Mei
4 mwaka huu akiwa kwenye ziara yake Mkoani Morogoro, Rais Magufuli
alibaini kero ya Mkandarasi kuchukua fedha kisha kushindwa kukamilisha
mradi wa maji katika kijiji cha Tundu Kata ya Kidodi, ambapo moja kwa
moja alimpigia simu Prof. Mkumbo na kumtaka kufika kijijini hapo.
Mei
5, Katibu Mkuu huyo wa Wizara hiyo alifika kijijini hapo na kutatua
kero hiyo ambapo tayari marekebisho ya mradi huo yameanza. Mradi huo
ulielezwa kukamilika lakini ukashindwa kutoa maji kama ilivyokuwa
imepangwa.
Pia
Prof. Mkumbo ameunda timu maalum ya watalaam watakaopitia upya usanifu
wa mradi huo na kuchukua hatua stahiki kwa wahandisi na mtaalam mshauri
aliyesanifu mradi huo.
Mbali
na hayo pia Katibu ametoa namba maalum kwaajili ya kurahisisha
mawasiliano kwa wananchi wenye kero za Maji waweze kuwasiliana naye moja
kwa moja ili aweze kushughulika na kero zao.
Post a Comment
karibu kwa maoni