0

Image result for KAMANDA MURILO 
Jeshi la polisi Mkoa wa Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam limeeleza kuwa watu watatu wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya Lori Scania  lenye namba za  usajili T 542 DA kuacha njia katika eneo la Boko MagengeniWilaya ya Kinondoni.
Mara baada ya ajali hiyo kutokea Dereva wa gari hilo alikimbia na jeshi la polisi linamsaka mtu huyo.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:00 jioni ya leo Mei 7,2018  baada ya gari hilo ambalo ni la mchanga kufeli breki na kugonga magari mengine ambapo watu watatu walifariki papo hapo.
Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa  Kinondoni,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo akizungumza na WALTER HABARI amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema watu watatu ambao wamepoteza maisha mpaka sasa bado hawajafahamika kwa majina.
Miili ya waliopoteza maisha imehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top