Na WAMJW-DSM
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeridhika na
maandalizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko ukiwemo
ugonjwa wa Ebola katika mipaka yote na viwanja vya ndege nchini
Hayo
yamesemwa jana na Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa ziara
yake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere
Dkt.Ndugulile
amesema amefika hapo ili kuangalia hali ya maandalizi na ufungaji wa
mashine za kisasa za utambuzi wa ugonjwa wa Ebola endapo itatokea mtu
mwenye ugonjwa huo
Aidha,
alisema wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa nchini na
kuweka mfumo wa kubaini watu wanaoingia kwa kubaini hali ya joto
linaloongezeka kwa mgeni anayeingia na kufanyiwa uchunguzi zaidi.
“tumeweka
mfumo wa kuwafuatilia wale ambao watakua wamebainika na joto zaidi
mahali watakapofikia na mawasiliano yao ili kujua hali zao na endapo
atapata mabadiliko”
Naibu
huyo aliongeza kuwa wamewafanyia mazoezi ya kutosha kwa watoa huduma wa
mipakani na viwanja vya ndege na pia kuwapatia elimu jinsi ya
kukabiliana na ugonjwa huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni