Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (Mb), amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara
kuwasilisha taarifa za takwimu za wazee ifikapo 30, Juni 2018.
Waziri
Jafo, alitoa kauli hiyo mapema jana alipokuwa akizindua zoezi la
kuwapatia vitambulisho maalum wazee wapatao 1,118 wa Jiji la Dodoma
kutoka kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru, Madukani, Makole na Majengo.
Vitambulisho hivyo, pamoja na mambo mengine vitawawezesha wazee hao
kupata huduma za afya bure na kwa wakati.
“Ifikapo
tarehe 15 Juni, 2018 kila kata iwe imetambua wazee na ifikapo tarehe 22
Juni, 2018 kila Halmashauri iwe imeunganisha taarifa za wazee kutoka
katika kata zake zote” alisema Waziri. Aidha Waziri Jafo aliagiza kuwa,
“ifikapo Juni, 26, 2018 kila Mkoa uwe umeunganisha taarifa zote na
kuzituma kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI”. Aliwaonyawale wote
watakaoshindwa kutimiza agizo hilo kuchukuliwa hatua kulingana na
miongozo, kwasababu watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndugu Godwin Kunambi
akizungumza katika hafla hiyo alisema shabaha ni kuwafikia wazee wote
kwenye Jiji hilo, na kubainisha kwamba, vitambulisho wanavyo vitoa kwa
wazee hao vitatumika pia kuwapa kipaumbele wazee sehemu zote za kutolea
huduma hususan ofisi za serikali.
“Mhe.
Waziri tunataka vitambulisho hivi tunavyo wapatia wazee wetu leo
viwasaidie pia kupata huduma kwa haraka na kwa wakati pindi wanapofika
kwenye ofisi zingine za Serikali” alisema Kunambi.
Mbali
na kutolea ufafanuzi wa matumizi ya vitambulisho hivyo, Mkurugenzi
Kunambi alisema juu ya Jiji hilo lilivyo jipanga katika suala zima la
makusanyo ya mapato ya ndani, ambayo ndio yamekuwa chachu ya kuboresha
huduma za afya kwa makundi maalum hususan wazee.
“Mhe.
Waziri, Jiji limepanga kukusanya Bil. 68 katika mwaka wa fedha ujao
ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha ambapo tulijiwekea lengo la
kukusanya Bil. 20 nahadi kufikia mwezi Februari tulikuwa tumekusanya
Bil. 14”. Kunambi ameongeza kuwa, katika mwaka ujao wa fedha wametenga
kiasi cha Mil. 58 kwaajili yakuwezesha huduma za wazee kwenye Jiji hilo.
Naye
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa Mhe. Deo Ndejembi, ametumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya
watendaji wanao waambia wazee kwamba hakuna dawa.
“Kumekuwepo
na malalamiko mengi siku za nyuma kutoka kwa wazee kuwa, baadhi ya
watendaji wa afya wanawanyanyapaa wazee na kuwaambia hakuna dawa
wafikapo vituoni, sasa Mhe Waziri, mimi niliseme kwa uwazi kabisa hatuta
mvumilia mtu yeyote atakaye onekana ni kikwazo kwa wazee hawa kadi
zimetoka wazee wahudumiwe, sio mnajiwekea vijiduka karibu na vituo
halafu mnawaambia waende waka nunue” alionya Ndejembi
Awali
akitoa taarifa ya uandaji wa vitambulisho Mganga Mkuu wa Jiji la
Dodoma, Dkt. Mohamed Nyembea, alisema utekelezaji wa zoezi hilo ulianza
kwa hatua za awali kwa kuwatambua wazee katika Kata 41 za Jiji la
Dodoma, ambapo jumla ya wazee 15,885 kutoka kata 33 miongoni mwa 41
wamekwisha tambuliwa na miongoni mwao wanawake ni 9,132 na wanaume ni
6,753 ambapo ni sawa na asilimia 80.5 ya kata zote 41 za Jiji la hilo.
Utoaji
wa vitambulisho kwa wazee ni utekelezaji wa sera ya Taifa ya wazee ya
mwaka 2003 ambapo inazungumzia mambo muhimu ya wazee ikiwepo kutenga
dirisha maalum katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Post a Comment
karibu kwa maoni