Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, mapema leo
amemkabidhi mwanafunzi wa kidato cha kwanza Nundoka Msangi, kiasi cha
shilingi milioni 3, kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya Sekondari
Mangula mkoani Morogoro.
Tukio
hilo limefanyika wilayani Mikumi mkoani Morogoro, ambapo Rais Magufuli
alisimama katika kijiji cha Mangula kwaajili ya kuongea na wananchi
waliokuwa wamesimama wakati wa msafara wake akielekea Wilayani
Kilombero.
Baada
ya kutoa hotuba fupi, Rais Magufuli aliuliza endapo shule ya sekondari
katika eneo hilo ina changamoto yoyote, ndipo kijana Nundoka akajitokeza
na kusema hawana vyoo na Rais akachangia milioni tatu na kuwataka
wanacnhi kushiriki katika ujenzi wa vyoo hivyo.
''Namkabidhi
hii pesa kijana Msangi, naomba zitumike vizuri kwenye ujenzi wa vyoo na
niwaombe tu wananchi mshiriki vizuri kujenga vyoo hivyo, nitarudi tena
kukagua,'' amesema Rais Magufuli wakati akikabidhi fedha hizo.
Magufuli
yupo Mkoani Morogoro akiendelea na ziara yake ya siku tatu ambayo
inahusisha uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Baadae leo
atazindua daraja la Mto Kilombero Mkoani humo.
Post a Comment
karibu kwa maoni