0

Ndg. Yassini Mohamed Kasiga wa wilaya ya Mvomero, kata ya Sungaji, kijiji cha Komtonga, kitongoji cha Digogo mwenye mahitaji maalumu akiweka alama za vidole kwenye mashine ya Usajili (Mobile Enrollment Unit - MEU) alipofika katika kituo cha Usajili kichangani Kusajiliwa ili apatiwe Kitambulisho cha Taifa.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeendelea kutoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalum, wazee, wajawazito na wenye watoto wachanga wanapokuwa katika foleni kuelekea kwenye chumba cha Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

Hilo limedhiirika pia kupitia shuhuda Ndg. Yassini Mohamed Kasiga wa wilaya ya Mvomero, kata ya Sungaji, kijiji cha Komtonga, kitongoji cha Digogo ambaye amezungumza akiwa amejawa na furaha akieleza kufurahishwa kupewa kipaumbele katika foleni ya kuelekea kwenye chumba cha Usajili. 

‘Ninaishukuru NIDA kwa kuweka utaratibu mzuri wa kutukumbuka wenye mahitaji maalum na kutupa kipaumbele cha kutopanga foleni muda mrefu ili tusajiliwe na kuwa na Kitambulisho cha Taifa kitakachotusaidia kupata stahiki zetu kirahisi kwani sasa tutatambulika kupitia Kitambulisho hicho.

Afisa Msajili (DRO) wilayani Mvomero Ndg. Kisa Moses Mwampeta ameeleza kuwa zoezi limeshakamilika katika tarafa ya Mvomero ambapo kwa sasa linaendelea kwa wananchi wa tarafa ya Turiani ndipo zoezi hilo lielekezwe kwenye tarafa nyingine mbili zilizosalia za Melela na Mlali, wilayani mvomero mkoani Morogoro.

Afisa Msajili (RO) wilayani Mvomero Bi Amina Mhando, akitoa maelekezo kwa Afisa Msajili Msaidizi (ARO) wakati zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu lilipokuwa linaendelea katika Kitongoji cha Dunduma.
Kwa upannde wake Msimamizi wa Kituo cha Usajili kata ya Mhonda, kijiji cha Kichangani amesema mwitiko wa wananchi katika kituo ni wa kuridhisha kuwawezesha vijana wake kuchapa kazi hadi jioni ili kuhakikisha wanasajili wananchi waliojitokeza kwa kasi kufikia lengo la kuwamaliza wananchi pindi muda uliotengwa unapowadia.
Ndg. Jackson Joseph Afisa Msajili Msaidizi wa NIDA, akigawa fomu zilizojazwa na wananchi wa kijiji cha Komtonga kwa ajili ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top