Akizungumza
na Manyara Fm ofisini kwake leo kamishna msaidizi wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Longinus
Tibishubwamu ameeleza kuwa kwa kipindi
cha mwezi mmoja hawajapata tukio lolote la uhalifu na kwamba jeshi hilo kwa
kushirikiana na wananchi linaendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu.
Akizungumzia
hali ya usalama bara barani amesema kuwa madereva boda boda wanaongoza kwa kuto
tii sheria za bara barani kwa kutovaa kofia ngumu,kubeba abiria zaidi ya mmoja
[mishikaki] licha ya kupatiwa elimu mara kwa mara na jeshi hilo.
Hata hivyo
Tibishobwamu amewataka wakazi wa Manyara kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo
vya ulinzi na usalama ili mkoa uendelee kubaki katika hali ya usalama.
Post a Comment
karibu kwa maoni