Wakazi wa
mtaa wa mruki mjini Babati wameuondoa madarakani uongozi mzima wa serikali ya
mtaa kwa madai kuwa wameshindwa kuwasimamia kikamilifu huku tuhma nyingi
zikienda kwa mwenyekiti Wilson Mtatiro.
Ni wale waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014.
Hayo
yamefikiwa jana mei 22 katika mkutano uliofanyika katika mtaa huo uliopo kata
ya Maisaka uliosimamiwa na katibu tarafa wilaya ya Babati kwa niaba ya Mkuu wa
wilaya Mhandisi Raymond Mushi, ambapo wananchi hao walikubaliana kupiga kura za
aina mbili,Waondoke au Wabaki,kura zaidi ya 130 zilisema Waondoke na 37
zilisema wabaki.
Baadhi ya tuhuma
zilizotajwa na wananchi hao dhidi ya mwenyekiti wao nai pamoja na Ukataji wa
miti na kuuza,kuuzia kokoto wakazi wa mtaa,kuuza ardhi ,uongozi kukosa utetezi
kwa wananchi wake na ubinafsi.
Akijibu
tuhuma hizo Mwenyekiti Wilson Peter Mtatiro amesema ‘licha ya kujitetea mbele
ya wananchi hao lakini wameamua kuniondoa’ila mimi sina shida,kwanza nimetumia
fedha zangu nyingi sana tangu niingie nkwenye System ya Serikali,hata mimi
nilichoka,nitaendelea kufanya biashara zangu.
Erick
Lema mjumbe wa kamati ya mtaa
aliejiuzulu kabla ya maamuzi ya wananchi yeye anasema hata katika mikutano
mwenyekiti hataki kusikiliza hoja za wenzake hali iyokuwa ikizua mtafaruku na
hata kutaka kupigana.
Diwani wa
Viti maalum[ CHADEMA] Babati mjini Plaksidia Claudi amesema kuwa kilichofanyika cha kuwqaondoa madarakani viongozi hao ni
uonevu mkubwa na kwamba ni wa kupangwa.
Wananchi
wamesema kuwa wamechoshwa na tabia za Mwenyekiti huyo kwa muda mrefu kwa
vitendo vyake alivyokuwa akivifanya ikiwemo dhuluma.
“Huu uongozi
kupitia mwenyekiti umekuwa ni wa dhulma,mimi mwenyewe nayeongea hapa
kanidhulumu elfu hamsini na tano niliyotumia nguvu zangu kuchimba mashimo ya
nguzo za umeme wa Rea,nilivyofuata pesa zangu akanijibu nionyeshe
tulipoandikishana kama unanidai” Alizungumza kwa uchungu Kijana Hasan Abdulmarik.
Post a Comment
karibu kwa maoni