Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA), kuacha kutumia lugha chafu na nguvu katika ukusanyaji wa kodi kwa
wafanyabiashara.
Pia
amemwagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kukutana na
uongozi wa mamlaka hiyo ili kuieleza umuhimu wa kuzingatia maadili na
weledi katika ukusanyaji wa kodi.
Majaliwa
ametoa maagizo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma, Frank
Mwakajoka aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu mbinu zinazotumiwa na
TRA kukusanya kodi kwa kuwatoza kodi kubwa isivyo halali wafanyabiasha
na wengine kupoteza maisha kwa mshtuko.
Mwakajoka
alisema licha ya serikali kutekeleza sera ya viwanda, TRA inatumia
mbinu za ovyo kukusanya kodi hali inayowalazimisha baadhi ya
wafanyabiashara kuhamishia biashara zao nje ya nchi.
Akijibu
swali hilo, Majaliwa alisema aliwahi kutoa maelekezo kwa TRA kutotumia
nguvu na kubambikia kodi kubwa na kwamba iwapo wafanyabiashara watakuwa
wana malalamiko, inabidi wayafikishe kwenye chombo cha kusikiliza
malalamiko kilichopo ndani ya TRA.
“Lakini
pia kama inapoonekana ndani ya TRA husikilizwi wizara ya fedha ipo na
ndio yenye mamlaka na TRA yenyewe, wafanyabiashara pia wana uhuru mkubwa
wa kwenda kwa kiongozi mkuu wa eneo mkuu wa mkoa kwenye hilo ngazi
mkoa au mkuu wa wilaya ngazi ya wilaya ili kulalamikia jamnbo hili na
hatimaye mkuu wa mkoa unachukua hatua kujua kwanini kumejitokeza katika
jambo hili.
“TRA
fanyeni kazi yenu kwa weledi, endeleeni kuwa na mazungumzo na
wafanyabiashara na sasa tunaona kila mmoja anaona umuhimu wa kulipa
kodi,” amesema Waziri Mkuu.
Post a Comment
karibu kwa maoni