0

Tafrani imezuka nchini India na kupelekea leo May 5, 2018 jeshi la polisi nchini humo kuwakamata wanaume 14 kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 16 na kisha kumchoma moto hadi kifo.

Inaelezwa kikundi hicho cha wanaume kilimteka binti huyo na kumpeleka porini kisha kumbaka.

Siku chache baada ya tukio hilo, baba mzazi wa binti huyo alikwenda kulalamika kuhusu tukio hilo kwenye ofisi za halmashauri.

Ofisi hizo ziliwaita vijana hao na kuwaamuru walipe faini ya Dola za Marekani 750 sawa na Shilingi za Kitanzania milioni 1.8 pamoja na kufanya ‘situps’ 100 kila mmoja wao.

Kutokana na adhabu hiyo, kikundi hicho kilikwenda nyumbani kwa binti huyo na kuwapiga ndugu zake na kisha kummiminia mafuta ya taa msichana huyo na kumuwasha moto.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top