0
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi.

POLISI mkoani Mara inamshikilia Benjamin Morati (49) mkazi wa Kijiji cha Nyabuzuma Tarafa ya Chamriho wilayani hapa, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake na kumficha ndani ya chumba cha kuhifadhia mahindi nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi alisema Morati anatuhumiwa kutenda kosa hilo Agosti 8, mwaka huu.
Kamanda Ng’anzi alimtaja kijana aliyeuawa kuwa ni Victor Benjamin (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kiroleli iliyoko wilayani hapa, ambaye alikutwa akiwa ameuawa na baada ya uchunguzi wa kitabibu alikutwa na jeraha kubwa kichwani lililotokana na kupigwa na kitu kizito.
Alisema mama mzazi wa kijana huyo alikuwa ameondoka siku moja kabla ya tukio hilo kutokea na kwenda katika wilaya ya Butiama kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za msiba na kumuacha kijana huyo na baba yake nyumbani hapo.
Aidha, alisema baba yake naye aliondoka katika mazingira ya kutatanisha nyumbani hapo na baadaye mwili wa kijana huyo ulikutwa katika chumba kinachotumika kama stoo ya kuhifadhia mahindi ndani ya nyumba yao.
“Tunamhoji baba wa marehemu kwa sababu aliondoka nyumbani hapo katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top