0

 
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe.
Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu kukataza mikutano yote ya ndani na nje  ya kisiasa mpaka pale watakairuhusu tena na kusema kwamba inatokana na sababu za kiupelelezi zinazoendelea na zitakapokamilika mikutano hiyo itaendelea.
Waziri wa katiba na sheria Dk. Harrison Mwakyembe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari baada ya kutoka kwenye hafla ya kuwaaga askari waliouawa juzi wakiwa wanajiandaa kutoka kazini iliyofanyika Kilwa Road akiiwakilisha wizara yake.
Kuhusu rais Magufuli kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na kuwahimiza watu kufanya kazi kwa ustawi wan chi,mwakyembe ambaye ni waziri mwenye dhamana ya katiba na sheria anasema kuwa rais hajapiga marufuku siasa alichokifanya ni kudhibiti uendeshaji huria/holela wa siasa nje ya maeneo yetu ya uchaguzi na ameafanya hivyo kuepusha shari.
Amewataka watanzania waiamini serikalia yao ya awamu ya tano inayosimamaiwa na RaisDk.Joseph Magufuli kwani anayo nia njema sana kwa kuwa ameweka mbele maslahi ya taifa hili na maslahi ya mnyonge bila kujali chama chochote.
“Hata sisi wasaidizi wake anakwenda mbali kiasi kwamba mpaka tunasema Mungu wangu wee hajifikirii hata yeye mwenyewe”.
Amesema kuwa waliopanga kufanya maandamano ya UKUTA septemba mosi ni kujitafutia matatizo yasiyo na maana akieleza kwamba dhamira yaserikali ni njema,Maandamano hayana tija,kama kuna sera unaona haijakaa vizuri milango haijafungwa ipo wazi na rais hajibiwi kupitia vyombo vya habari  wala maandamano bali upo utaratibu.

Mwakyembe amehusisha tukio hilo la mauaji ya askari hao wanne  na visa vya kisiasa.”Sasa kufuatia tukio hilo baya ambalo ukiangalia mazingira yake yote lengo lilikuwa ni kuwaua  hao polisi kwa sababu bank ilikuwepo karibu lakini hawakupora pesa  na kupora silaha,lakini vile vile na viashiria vingine vya kisiasa vyenye shari,  jeshi letu la polisi ambalo linabeba wajibu kisheria kulinda amani ya nchi hii limekuja na hiyo amri ya muda kutokana na hali halisi iliyopo kwamba ebu tusitishe hata vikao hivyo vya ndani,na mimi kama waziri wa Katiba na Sheria nasema hiyo ni amri halali na inapaswa kuzingatiwa, kutiiwa na kila chama cha siasa bila ubaguzi’.
 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top