0
Watu watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya gari moja lililokuwa katika msafara wa makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuacha njia na kupinduka kati ya kijiji cha NANGURUWE na MALANJE mkoani MTWARA.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa TBC MARTINA NGULUMBI msafara huo ambao ulikuwa ukitokea mjini MTWARA kwenda wilaya ya TANDAHIMBA ambako Makamu wa Rais SAMIA anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani humo.
MARTINA amesema majeruhi wa ajali hiyo waliopelekwa hospitali ya rufaa ya  mkoa wa MTWARA, LIGULA kwa matibabu wote wanatoka ofisi ya makamu wa rais.
Msafara huo wa makamu wa rais  umeshawasili wilayani TANDAHIMBA ambako Makamu wa Rais SAMIA anatarajiwa pamoja na mambo mengine kukagua viwanda vya kubangua korosho na kuzungumza na wakazi wa mkoa wa MTWARA kupitia mkutano wa hadhara utakaoufanya wilayani humo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top