0
Wanafunzi katika shule za msingi wanakabiliwa na tatizo la minyoo inayochangia kuzorota kwa afya na udumavu wa akili hali inayosababisha maendeleo duni ya kitaaluma.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mazoezi iliyoko wilayani Monduli Prisila Moses amesema kuwa tatizo la minyoo kwa wanafunzi limekuwa likisababisha wanafunzi kusinzia darasani ,kudhoofika kiafya na kushindwa kufuatilia masomo kwa umakini.
Afisa Masoko wa Shirila la Afya la AAR, Daudi Boaz.
Abigaeli Ronald na Ezra Ibrahim ambao ni Wanafunzi katika Shule hiyo wamesema kuwa kuna uhitaji wa watoto kupatiwa dawa za minyoo ili kuwa na afya bora itakayowawezesha kufanya vizuri kitaaluma tofauti na hali iliyoko hivi sasa.
Daudi Boaz ni Afisa Masoko wa Shirila la Afya la AAR lililotoa dawa za minyoo shuleni hapo pamoja na kupanda miti amesema kuwa utoaji wa dawa hizo utasaidia ustawi wa afya za wanafunzi pamoja na masomo kwani minyoo ina madhara makubwa kwenye afya ya mtoto na kumfanya adhoofike kwa kupungukiwa na virutubisho mwilini ambavyo huliwa na minyoo.
Zoezi la Ugawaji wa dawa za minyoo kwa watoto wa Shule ya Msingi Mazoezi iliyoko katika wilaya ya Monduli limefanyika huku likiambatana na shughuli za upandaji miti ili kuboresha mazingira na afya.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top