0

BABATI MANYARA
 Baadhi ya wapiga matofali, wajenzi na watumiaji wengine wa saruji mkoani Manyara walioudhuria mafunzo ya utengenezaji wa matofali bora na matumizi sahihi ya saruji yaliyoendeshwa na Simba Cement karibuni.  Mafunzo kama hayo yamefanyika pia katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Singida na Dodoma.

Serikali imeombwa kushusha gharama za nishati ili bidhaa mbalimbali hapa nchini viwanda vinavyozalisha bidhaa mbali mbali ziweze kuuzaa bidhaa  zao kwa kwa bei wananchi watakazoweza kuzimudu.

Hayo yameelezwa na meneja wa mauzo wa kampuni ya saruji ya tanga sementi taifa bw;leslie masawe katika semina ya siku1 kwa wadau wa ujenzi mjin babati mkoani manyara.

Hata hivyo bw masawe amesema kwa sasa kiwanda hicho kinatumia nishati ya joto ya makaa ya mawe ambayo inapatikana mkoani iringa umbali wa km zaidi ya 200 suala ambalo bado ni changa moto kubwa kwa kiwanda hicho.

Aidha ameoeongeza kuwa endapo serikali ingefikisha nishati ya gesi mkoani Tanga ingekuwa vyema na uafadhali kwani wangetumia nishati hiyo katika uzalishaji kiwandani hapo na kupunguza gharama za uendeshaji.

Kauli hiyo inakuja huku serikali kupitia TPDC ikiwa tayari imeshaweka mkakati wa kusambaza mabomba ya gesi asilia ambayo pia kwa kaskazini  litapita mkoani Tanga.

Akitoa semina ya siku moja mhandisi wa Petroli Tanzania [TPDC] Felix Nanguka ameeleza kuwa mradi huo wa gesi asilia serikali itakuwa na asilimia 20 akiwa kama mshirika.

Kwa Tanzania ugunduzi wa Gesi asilia  mpaka sasa ni Trioni 57.25% nyingi ikiwa ni kutika katika ukanda wa Maziwa na Bahari.

Hata hivyo  kampuni ya Tanga sementi imeanzisha bidhaa mbalimbali  mpya za simenti huku hivi sasa ikiingiza simenti yenye ujazo kama ule wa Simba siment yenye jina Mkombozi simenti ya  mwendo kasi yenye ubora  na  gharama nafuu inayoendana na maisha ya Mtanzania pamoja na nyingine ambayo ni mahususi kwa ajili ya ujenzi wa bara bara.

Katika mafunzo hayo Masawe aliwafundisha wadau hao wa Saruji mkoa wa Manyara  mbinu  za ujenzi kwa kutumia sementi vizuri ili kuepuka kupasuka na kubomoka kwa nyumba nakuongeza kuwa uzingatiaji viwango vya ujenzi ili kuepusha kubomoka kwa nyumba hata kipindi cha maafa kama ya tetyemeko la ardhi kama yaliyovyotokea huko mkoani Kagera na kusababisha nyumba nyingi kubomoka.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top