Jeshi la polisi mkoani Arusha linawaashikilia watuhumiwa 14 na jumla ya
kete 167 za madawa ya kulevya aina ya HEROIN. Mbali na watuhumiwa hao wa
madawa ya kulevya misako hiyo ilifanikisha kukamata madawa ya kulevya
aina ya mirungi kilogram 33 pamoja na watuhumiwa 12
Kamanda wa polisi ameeleza kuwa tangu kuanza mwezi huu wa pili jeshi
la polisi limekuwa likifanya misako mbali mbali katika Bara Bara, mitaa
na vitongoji mbali mbali ndani ya wilaya zote za mkoa wa Arusha
ambapo jumla ya misokoto 3845 ya bangi ilipatikana na jumla ta
watuhumiwa 54 walikamatwa na kufunguliwa kesi katika vituo mbali mbali
vya polisi.
Kati ya watuhumiwa hao waliokamatwa na Bangi Kuna wauzaji wa madawa hayo
ambapo idadi Yao Ni 40, msafirishaji mmoja na Askari mmoja kwenye namba
za kijeshi F.6978 D/CPL ZAKAYO ambae nae anashikiliwa huku uchunguzi
dhidi yake ukiendelea kufanyika.
Jumla ya watuhumiwa 12 wa mirungi na 14 wa heroin wote wana makosa ya
kupatikana na madawa hivyo kufanya jumla ya watuhumiwa wote kufikia 80.
Post a Comment
karibu kwa maoni