0
BENNY MWAIPAJA-WFM, DAR ES SALAAM

Image result for makamu wa rais benki ya maendeleoMAKAMU wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB, Bw. Amadou Hott, ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu ili iweze kutekeleza malengo yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda katika kipindi kifupi kijacho.

Bw. Amadou Hott, anayeshughulikia masuala ya Nishati na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, amesema Benki hiyo imetenga kiasi cha Dola Bilioni 12 kuzisaidia nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ili ziweze kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na vitendo vinavyochangia mabadiliko ya Tabia Nchi.

Amemweleza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alipokutana na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwamba kipaumbele kikuu ni kuhakikisha kuwa sekta ya Nishati inaboreshwa hapa nchini kwa kuhuisha Shirika la Ugavi wa Umeme nchini-TANESCO kuondokana na madeni makubwa yanayolikabili,  ili liweze kuchochea uchumi na ukuaji wa viwanda kwa kutoa huduma bora na kwa gharama nafuu.

Pause

Amesema kuwa Benki yake pia imekuja na mkakati wa kuhimiza matumizi ya nishati jadidifu ili kupunguza ama kuondoa kabisa matumizi ya kuni katika kupikia badala yake matumizi hayo yaelekezwe katika kutumia nishati mbadala ili kuokoa kiasi kikubwa cha miti na misitu inayoharibiwa nchini ambapo watafadhili miradi ya matumizi ya nishati mbadala katika maeneo ya mijini na vijijini

Pause

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, pamoja na mambo mengine, amepongeza jitihada za Benki hiyo katika kuboresha miundombinu ya barabara hapa nchini na amemwomba Makamu huyo wa Rais wa AfDB kusadia ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa, hatua ambayo itachangia kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika eneo lote la maziwa makuu

Pause

Mkutano kati ya Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Bw. Amadou Hott na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, umehudhuriwa na maafisa waandamizi wa Benki hiyo pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top